MWANAMKE ALIYESHINDA KITI CHA URAISI KWA MARA YA PILI
Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa urais nchini Brazil 2011, Diana Rousseff amechaguliwa tena kushika wadhifa huo katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili Oktoba 25 nchini humo.Baada ya kutangazwa kushinda katika kinyang’anyiro hicho, Rousseff mwenye umri wa miaka 66 amesema anahitaji kufanya vizuri katika awamu hii ya uongozi wake huku akisifia jitihada zake na rais aliyemtangulia Luiz Inacaio Da Silva kuwa katika vipindi vyao vya uongozi wametatua tatizo la ajira kwa kiasi kikubwa. Rousseff ameshinda kwa 51.59% ambapo mpinzani wake Aecio Neves amepata kura 48.41%