MUME WA FROLA MBASHA ATUHUMIWA KUMBAKA SHEMEJI YAKE
Dar
es Salaam.Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, anatuhumiwa
kumbaka shemeji yake mdogo 17.Taarifa za tukio hilo ziliripotiwa juzi
saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule), zikimtuhumu
mwanamume huyo kwamba alimbaka binti huyo mara tatu na kumsababishia
maumivu makali.
Binti
huyo alifika katika kituo hicho cha polisi akiwa na ndugu zake wawili
ambao walilalamika kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kutoka upande wa
mtuhumiwa wa kuzima kesi hiyo.
Akizungumza
na blog hili nje ya kituo hicho, binti huyo alisema shemejiye alimbaka
mara ya kwanza, Ijumaa iliyopita na Jumapili alipombaka mara mbili ndani
ya gari.
Alisema
mara ya kwanza alikaa kimya baada ya mtuhumiwa kumtishia kwamba
angemdhuru kama angetoa taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa wakiwa
sebuleni nyumbani kwako Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa taarifa kwa
ndugu zake baada ya kubakwa mara ya pili.
Polisi
katika kituo hicho walithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo lakini
walishindwa kwenda kumkamata mtuhumiwa kwa maelezo kwamba hawakuwa na
askari wa kutosha na kuahidi kwamba angekamatwa jana. Hata hivyo, hadi
jana mtuhumiwa huyo alikuwa hajakamatwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi kutwa nzima ya jana
hakupatikana kuzungumzia tukio hilo na kila simu yake ilipopigwa (kati
ya saa nane mchana na saa mbili usiku), ilipokewa na msaidizi wake
akisema bosi wake ana kazi nyingine.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hakuwa amepokea taarifa yoyote ya aina hiyo.
Mwimbaji anena
Alipoulizwa
jana, mwimbaji huyo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia kwa undani
tuhuma zinazomkabili mumewe na kwamba alikuwa anajisikia vibaya kutokana
na tukio hilo kuhusisha watu wake wa karibu.
“Of
course (bila shaka), hili sio tukio zuri. Kwa sasa sina uwezo wa
kuzungumza kwa sababu hili suala lipo Polisi. I am confused
(nimechanganyikiwa), ukizingatia kwamba linasemekana kutokea wakati
sikuwepo nyumbani, naomba tuzungumze baada ya akili kutulia,” alisema.
Kadhalika,
jana saa 6:20 mchana, gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mtuhumiwa
ambaye baada ya kupewa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili alisema:
“Samahani sana ujue sikusikii kabisa,” kisha alikata simu.
SOURCE:SINTAH
Sijui ndo nyakati za mwisho, sijui ndo kupitiwa na shetan????
Mungu amuongoze na kumpa nguvu huyo mtoto.
Comments
Post a Comment