Emmanuel Mbasha na Mkewe :The Saga Continues
![]() |
Emmanuel Mbasha na mkewe |
Emmanuel
Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora
Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe
kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka
17.
Faili la tuhuma dhidi
ya Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi
Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina tunalihifadhi),
alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi
hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014.
Tangu siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa inamsaka Mbasha bila ya mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa huyo aliongea na gazeti hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na kwamba yuko tayari kujisalimisha ili ukweli ubainike.
“Tuhuma dhidi yangu ni
za kutengeneza,” alisema Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana
na mgogoro wa kifamilia baina yake na Flora na familia yake ambao
alisema umedumu kwa siku kadhaa.
“Mimi sijabaka na
sijawahi kubaka; sijatenda dhambi yoyote; sijafanya kitu chochote na
kibaya haya mambo yote ni ya kusingiziwa tu. Mungu wangu ni shahidi. Na
kwa kuwa sijafanya hiyo dhambi kama wanavyodai, basi Mungu wangu
atanitetea,” alisema Mbasha ambaye anaonekana zaidi kwenye video ya
wimbo wa Maisha ya Ndoa alioshirikiana na mkewe Flora.
Kabla
ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo, msichana huyo alipelekwa
Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana) ambako alifunguliwa faili
la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo ambavyo vilifanywa na daktari
kung’amua kama binti huyo aliingiliwa vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu
utokaji wa mbegu usio wa kawaida (HVD).
Kadhalika binti huyo
alifanyiwa vipimo kuona kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi (VVU), pia
kupata ujauzito, lakini matokeo ya awali yalionyesha kuwa yupo salama.
Akiwa nje ya kituo cha
polisi Jumatatu usiku, binti huyo aliliambia gazeti hili kwamba mara ya
kwanza alibakwa mchana Mei 23 na kwamba mtuhumiwa alirudia kitendo
hicho Jumapili Mei 25 usiku ndani ya gari katika eneo la Tabata, ambako
anadai alifanyiwa kitendo hicho mara mbili.
Hata hivyo, Mbasha
alihoji: “Hivi kweli hata kama mimi ni mbakaji, kweli nimbake mtoto wa
kumlea mwenyewe mara tatu, yaani Ijumaa halafu nirudie tena Jumapili?
Hata kama ni kusingiziwa basi tuhuma hizi zimezidi.”
“Huyu binti nimekaa
naye miaka mingi na sijawahi kumfanyia hivyo. Hapo nyumbani kwangu
wamekaa mabinti wengi, wakiwamo shemeji zangu wadogo zake na Flora na
sikuwahi hata kuwagusa, leo hii kwa nini wananifanyia hivi?”
Courtesy:Sintah
Comments
Post a Comment