MARTIN KADINDA AFUNGUKA KUHUSU HISIA ZAKE ZA KIMAPENZI KWA WEMA SEPETU


MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda amesema kabla hajawa kiongozi wake, awali aliwahi kumtamani kimapenzi mcheza filamu Wema Sepetu, lakini alighairi baada ya kugundua ni mwanamke wa kudekadeka.Kadinda alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akihojiwa kwenye kipindi cha sporah show kuhusu masuala mbalimbali yanayomhusu msichana huyo ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
Martin Kadinda akiwa na Wema Sepetu.
 Kuhusu maisha wanayoishi nyota hao wawili wapenzi, Kadinda alisema kwa jinsi wanavyoishi ni kama watu wanaoigiza, akitolea mfano wa kipindi walichorudiana wakiwa nchini China, ambako wenyewe walisema wanaigiza filamu wakati ndiyo kwanza walikuwa wanarejesha penzi lao lililovunjika mara ya kwanza.

Comments

Popular posts from this blog

10 Celebs Who Killed Their Careers After Dissing Beyonce

65 Home Business Ideas You Can Do From Your Kitchen Table

Top 7 Must Watch Tv Shows about Money and Business