Rais Uhuru Kenyatta na Akon nchini Marekani.

Uhuru na Akon 1
Hapa walikutana wakati wa mapumziko kwenye hili kongamano
Rais  Uhuru Kenyatta wa Kenya ni miongoni mwa Marais wachache wenye umri mdogo kulinganisha na Marais wengi ambapo amekua akienda sawa na baadhi ya mahitaji au tabia ya vijana wengi ikiwemo kujumuika na Wasanii wakubwa hata wa Kenya kama Jaguar ambae huwa mara nyingi anakuwepo kwenye hafla za Ikulu..



Hizi picha zake za Marekani kwa mujibu wa ripota wa Kenya Julius Kepkoich, ni kwamba mmoja wa Waandaaji wa mkutano wa Brook Business uliowakutanisha pamoja marais wa afrika na wakuu wa kampuni za kimataifa ni mwimbaji Akon.
akon 12
Akon mwenye asili ya Senegal aliezaliwa miaka 41 iliyopita ni miongoni mwa wakali wachache kutoka Afrika ambao waliweza kupenda na kuingia kwenye chati za muziki wa dunia.
Pamoja na umaarufu na utajiri wake alioupata akiwa anaishi mpaka sasa nchini Marekani, Akon bado ameendelea kuikumbuka Afrika na hata kwenye baadhi ya interview zake na anachoandika kwenye mitandao ya kijamii, anasisitiza watu kuwekeza Afrika.
Uhuru na Akon 2Credit: Matukio na Vijana

Comments

Popular posts from this blog

10 Celebs Who Killed Their Careers After Dissing Beyonce

65 Home Business Ideas You Can Do From Your Kitchen Table

Top 7 Must Watch Tv Shows about Money and Business