AL-SHABAAB WAKIRI KIFO CHA KIONGOZI WAO!

Wapiganaji wa Al-shabaab
Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab limethibitisha kuwa kiongozi wake Ahmed Abdi Godane aliuawa siku ya jumatatu katika shambulizi la angani lililotekelezwa na wanajeshi wa Marekani. 

Msemaji wa Alshabaab amesema kuwa wanachama wengine wawili wa kundi hilo pia walifariki katika shambulizi hilo ,yapata kilomita 170 kusini mwa mji mkuu wa Mogadishu.


 

Ripoti zinasema kuwa kundi la Alshabaab limemchagua kiongozi mpya Ahmad Omar,katika mkutano uliofanyika katika eneo lisilojulikana.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi amesema kuwa kiongozi huyo hafahamiki vyema.

Comments

Popular posts from this blog

10 Celebs Who Killed Their Careers After Dissing Beyonce

65 Home Business Ideas You Can Do From Your Kitchen Table

Top 7 Must Watch Tv Shows about Money and Business