MTOTO ALIYEOKOLEWA NA POLISI KENYA ALIKUWA ANAKUJA KUUZWA TANZANIA
Ni
pale ambapo unaweza kuvuta picha baba anajaribu kufanya mbinu za
kumsafirisha mtoto wake kwenda nchi ya pili ili akamuuze kwa watu ambao
ameshazungumza nao kabisa na wako tayari wanasubiria biashara ifanyike.
Yani hiki
kisa kilichotokea Kenya kina uzito wake mpana tu sababu Baba mzazi na
Baba wa kambo wote wamehusika kwa nyakati tofauti kufanya mbinu za
kutaka kumsafirisha mtoto huyu ambae ni Albino ili aje Tanzania kuuzwa
na viungo vyake vitumike kwa imani za kishirikina.
NTV wameripoti
kwamba Polisi wa Kenya ndio walimuokoa huyu mtoto akiwa tayari
ameshaingizwa Tarime Tanzania akiwa anasafirishwa kwa siri na baba yake
wa kufikia (wa kambo) ambapo mama mzazi amesema baada ya kuolewa na mume
wa pili baada ya kuachana na yule wa kwanza ambae ndio baba wa mtoto,
amekutana na kitu kilekile kama alichotaka kufanya mume wa kwanza, mume
wa pili pia anataka kumuuza huyu mtoto.
Mama wa
mtoto anasema ‘ninachoshangaa ni kwamba baba yake mzazi alipotaka
kumuuza huyu mtoto alikamatwa, tena baba yake wa pili amejaribu kuja
kutaka kuiba tena huyu mtoto, ni giza ambalo nimeliona kwangu na kuhofia
maisha ya mtoto na mpaka sasa tunamfungia ndani hawezi kutoka hata
kwenda shule’
Kwenye sentensi nyingine mama wa mtoto huyu anasema ‘Wakati
mwingine najiuliza kwa sababu baba yake mzazi wa kwanza alishikwa na
Polisi lakini sijui hiyo kesi iliendeleaje na akaachiliwa, sasa ni kama
wameona ni kawaida hata kama wanakwenda kuripotiwa hakuna hatua yoyote
inachukuliwa kuhusu huyu mtoto’Ni pale ambapo unaweza kuvuta
picha baba anajaribu kufanya mbinu za kumsafirisha mtoto wake kwenda
nchi ya pili ili akamuuze kwa watu ambao ameshazungumza nao kabisa na
wako tayari wanasubiria biashara ifanyike.
Yani hiki
kisa kilichotokea Kenya kina uzito wake mpana tu sababu Baba mzazi na
Baba wa kambo wote wamehusika kwa nyakati tofauti kufanya mbinu za
kutaka kumsafirisha mtoto huyu ambae ni Albino ili aje Tanzania kuuzwa
na viungo vyake vitumike kwa imani za kishirikina.
Comments
Post a Comment