MABINGWA WA KUDANGANYA WHATSAPP, DAWA IMESHAPATIKANA!
Whatsapp wamewapunguzia sababu ya kujitetea wale wote wenye tabia za
kutojibu message kwa kisingizio kuwa hawakuziona hata kama zilionesha
tiki mbili kuashiaria zimefika. Sasa Whats App imeongeza alama ya
kuonesha kuwa ujumbe umesomwa na muda ambao umesomwa.
Kabla ya maboresho hayo kulikuwa na aina mbili tu za tiki, tiki moja
ya kijivu ilikua ikionesha ujumbe umetumwa, tiki mbili za kijivu
ziliashiria ujumbe umefika.
Upande wa messages za group, tiki mbili za blue zitakuwa zikionekana pindi tu watu wote kwenye group wakiusoma ujumbe.
Ili kuona mabadiliko hayo, mtumiaji wa Whatsapp anapaswa ku update app hiyo kwenye simu yake.
Comments
Post a Comment