MAREKANI: WAZIRI WA ULINZI CHUCK HAGEL AJIUZULU
Barack obama amekubali Jumatatu Novemba 24 ombi la kujiuzulu kwa waziri wake wa ulinzi, Chuk Hagel.
Waziri wa
ulinzi wa Marekani Chuck Hagel, amewasilisha barua yake ya kujiuzulu
Jumatatu Novemba kwenye Ikulu ya Washington. Kujiuzulu huko kumetangazwa
na Chuck Hagel wakati wa mkutano na vyombo vya habari, mkutano ambao
umehudhuriwa na barack Obama.
Kulingana na
kauli ya Barack Obama, Chuk Hagel ndiye ametaka mwenyewe kutamatisha
muhula wake kwenye wadhifa aliyokua akishikilia. Kati ya wawili hao
hakuna aliyetoa maelezo zaidi kuhusu uamzi huo wa kujiuzulu. Lakini kwa
mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, waziri wa ulinzi alikua
alipewa shinikizo.
Gazeti la
New York Times limebaini kwamba kujiuzulu kwa Chuk Hagel kunahusiana na
hali ya kutoelewana iliyojitokeza katika vita vinavyoendeshwa na
Marekani dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Iraq na
Syria.
Inasadikiwa
kuwa Ikulu ya washington huenda ilikua ikitathmini mkakati wake dhidi
ya wanajihadi na ilikua inahitaji mkakati huo uanze kutekelezwa na
waziri mpya wa ulinzi. Chuck Hagel awali alikuwa na wajibu wa kusimamia
uondoaji wa majeshi kutoka Iraq na Afghanistan, wala si kusimamia
operesheni ya kijeshi.
Washirika
wa karibu wa Barack Obama wamekanusha hoja ya kujiuzulu kutokana na
kushinikizwa. " Hakuna tofauti ya maoni ambayo imesababisha Chuk hagel
anachukua umazi huo wa kujiuzulu", maafisa wa Ikulu ya Washington
wamesema. Maafisa hao wamebaini kwamba mazungumzo ya kujiuzulu kwa Chuk
Hagel yalianza wiki mbili zilizopita.
Waziri wa
Ulinzi ataendelea kushikilia wadhifa huo hadi atakapopatikana mrithi
wake. Majina kadhaa tayari yameanza kutajwa, ikiwa ni pamoja na Michèle
Fournoy, aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi.
Comments
Post a Comment