NESI WA EBOLA ALIYEWEKEWA KARANTINI KUFIKISHWA MAHAKAMANI
Nesi Kaci
Hickox akiendesha baiskeli baada ya kuvunja karatini aliyowekewa wakati
akiwa kwenye uchunguzi wa Ebola baada ya kurudi toka Afrika Magharibi
alipokua akiwatibu wagonjwa wa Ebola
Mamlaka
ya afya mji wa Fort Kent, Maine uliopo mpakani wa Canada wamesema
watamfikisha mahakamani Nesi Kaci Hickox baada ya kuvunja karantini siku
ya Alhamisi Oktoba 30, 2014 kwa kutoka nje ya nyumba yake na kuendesha
baiskeli takribani saa moja.
Nesi Kaci
Hickox aliwekewa karantini hiyo baada ya kurudi toka Afrika Magharibi
alipokua amekwenda kuwatibia waathirika wa ugonjwa wa Ebola.
Pamoja na
ulinzi wa polisi uliowekwa nje ya nyumba yake Nesi Kaci Hickox
alithubutu kutoka nje ya nyumba yake kwa siku mbili mfulululizo baada ya
siku ya Jumatano Oktoba 29, 2014 kutoka nje ya nyumba yake na kuongea
na waandishi wa habari huku akishikana mkono na baadhi ya waandishi hao.
Nesi Kaci Hickox alitakiwa akae ndani ya nyumba yake kwa siku 21 mpaka Novemba 10
Comments
Post a Comment