RAIS OBAMA ASIFU UVAAJI WA FULANA YA I CAN'T BREATHE ALIYOVAA MCHEZAJI WA KIKAKPU LEBRON JAMES
Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama amesifia uvaaji wa fulana wa
mchezaji wa mpira wa kikapu Lebron James wakati alipokua akifanyiwa
mahojiano na gazeti la the people magazine. Rais Barack Obama alipouliwa
swali hilo nini mtizamo wake alisema nadhani ni jambo zuri kwa mchezaji
huyo na wengine waliopaza sauti zao kuwakilisha mawazo yao kwa mambo
yaliyotokea ya kuuwawa kwa Wamarekani weusi na polisi huko Ferguson
jimbo la Missouri na Brooklyn New York na baadae mahakama kuwaachia huru
polisi hao waliofanya mauaji hayo kwamba walikua wakitekeleza wajibu
wao wa kazi.
I can;t Breathe ni maneno ya mwisho aliyeongea Eric Garner kabla ya
kukata roho baada ya kukabwa koo na polisi wakati walipokua wamekwenda
kumtia mbaroni.
Comments
Post a Comment