Fahamu kiundani kugombana mpaka kupatana kwa P-Square




 


P Square hatimaye imerudi upya na kwa kasi. Lakini swali kubwa lilikua nini kilikua chanzo cha ugomvi wao? Ungana nami tuanzie kwenye chimbuko mwaka 2015.

Palianzaje (2015 to early 2021)

Peter na Paul wamesuluhishana ikiwa ni miaka zaidi ya mitano tangu PSquare kuvunjika, Huku tukio hili likiwa linahusishwa na sababu mbalimbali. 


Paul aka Rudeboy (Mwenye rasta) alidai kuwa chanzo cha wao kutengana kilikua sababu za kifamilia na hajawahi sema nini ilikua shida. 


Peter aka Mr. P. alisema kuwa sababu ya wao kugombana ni kutokubaliana katka maswali mbalimbali ya kimuziki ikiwa pamoja na shughuli hasa za kaka yao (Jude Engeez) kama meneja wao. Anasema kuwa kuna kipindi kaka yao alkua anakosa misimamo na maamuzi mazuri ya kimaslahi kwao, ndipo alipomuomba aache kazi ya kuwa meneja wao, ila pacha wao akamtetea sana kaka yao, na kaka yao akawa anatishia kumchapa vibao Peter. Anasema haikuishia hapo kuna muda Paul alikua nanafanya solo works. Na yeye Peter alikua bado anamsapoti na kutokea kwenye videos lakini yeye alkua akifanya solo works kaka ake hatokei wala kumsapotI. Visa viliendelea sana kati yao,, Kiasi kwamba waliacha kuongea December 2015. 


Kitaa kinasema kuwa Lola (Mke wa Peter) alikua chanzo cha group kutawanyika maana alikuja na ideas zake kwa Peter kwa namna gani Peter anaweza kukua kimziki ambazo hazikumhusisha Paul na watu kwa miaka zaidi ya mitano walimnanga sana binti kwa kuwa chanzo cha kundi kutawanyika na sababu nyingine kubwa ikiwa marehem mama yao hakumtaka binti kwa sababu ya ukabila na insticts, ikumbukwe Peter alimuoa mkewe miezi michache tu baada ya mama yake kufariki.  





Sasa (2021)


Mpaka August 2021 ambapo ilisemekana moja ya sababu ya Anita (mke wa Paul) kumuacha Paul ilikua ni Paul kusema anataka kuzika ugomvi na pacha wake na kundi lirudi. 


Mke wa Paul alibeba watoto wake na kwenda nao Marekani na kudai takribani Milion 30 (US$ 15,000) kwa mwezi kama child support na kudai watabak kama wazazi wenza kwa ajili ya watoto wao (Story ya juu ya chanzo cha talaka yao kwa undani zaid)





Mapema mwezi huu, Peter alionekana akiwatoa out kuwanunulia toys mbalimbali watoto wa Paul na watoto walionekana wenye furaha sana kutolewa na uncle wao ukiacha kununuliwa toys, jewellery na nguo. 


Haikuishia hapo, Peter na Paul, week hiyo hiyo wakaonekana kama ‘wamefollowiana’ tena Instagram, huku nderemo na vifijo vkatawala kwa fans wao, wengi wakisema “Hakuna Jambo lisilowezekana kwa Mungu”. 





Wiki hii wameonekana wakikumbatiana kwa pamoja ikiwa ni appearance yao ya kwanza wakiwa pamoja bila vita nene kati yao kwa zaidi ya miaka mitano. 


Leo ilikua birthday ya mastaa hao ambao wanafikisha miaka 40 na wamejipost kwa bashasha tele na kutoa account  number yao kama Davido alivyofanya jana, mpaka sasa hawajatoa mfafanua wa sh. Ngapi wamepokea ila tunajua ztakua nyingi sana kutokana na furaha ya wadau. 


Wadau tunasubiria banger la kufungia mwaka kutoka kwa PSquare. I am excited, are you?


 Leave a comment below or visit our Social Media pages linked below:

Instagram 24tz 

Facebook 24tz

Twitter 24tz


Comments

Popular posts from this blog

10 Celebs Who Killed Their Careers After Dissing Beyonce

TOP TEN PRIVATE JETS

10 Simple Things Remarkably Likeable People Do