Dar  es Salaam.Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili,  anatuhumiwa  kumbaka shemeji yake mdogo 17.Taarifa za tukio hilo ziliripotiwa juzi  saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule), zikimtuhumu  mwanamume huyo kwamba alimbaka binti huyo mara tatu na kumsababishia  maumivu makali.     Binti  huyo alifika katika kituo hicho cha polisi akiwa na ndugu zake wawili  ambao walilalamika kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kutoka upande wa  mtuhumiwa wa kuzima kesi hiyo.     Akizungumza  na blog hili nje ya kituo hicho, binti huyo alisema shemejiye alimbaka  mara ya kwanza, Ijumaa iliyopita na Jumapili alipombaka mara mbili ndani  ya gari.     Alisema  mara ya kwanza alikaa kimya baada ya mtuhumiwa kumtishia kwamba  angemdhuru kama angetoa taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa wakiwa  sebuleni nyumbani kwako Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa taarifa kwa  ndugu zake baada ya kubakwa mara ya pili...