MWANAMKE ALIYESHINDA KITI CHA URAISI KWA MARA YA PILI
 
                Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa urais nchini Brazil 2011, Diana  Rousseff amechaguliwa tena kushika wadhifa huo katika uchaguzi mkuu  uliofanyika siku ya Jumapili Oktoba 25 nchini humo.Baada ya kutangazwa  kushinda katika kinyang’anyiro hicho, Rousseff mwenye umri wa miaka 66  amesema anahitaji kufanya vizuri katika awamu hii ya uongozi wake huku  akisifia jitihada zake na rais aliyemtangulia Luiz Inacaio Da Silva kuwa  katika vipindi vyao vya uongozi wametatua tatizo la ajira kwa kiasi  kikubwa.       Rousseff ameshinda kwa 51.59% ambapo mpinzani wake Aecio Neves amepata kura 48.41%