Baada ya kuibuka na Tuzo ya AFRIMMA, Lady Jaydee kutua Bongo August 3
Lady
Jay Dee ambaye ameshinda tuzo ya AFRIMMA kama mwimbaji bora wa kike
Afrika Mashariki atatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere, Dar es Salaam, August 31 mwaka huu akitokea Marekani.Akiongea
na tovuti ya Times Fm, meneja wa Lady Jay Dee, Captain Gardener G.
Habash amesema kuwa mwimbaji huyo anatarajia kuondoka Houston, Marekani
August 1 na kuingia Dar es Salaam August 3.
Amesema Lady Jay Dee yuko Marekani alikuwa ameenda kwa ajili ya likizo au mapumziko.
Tuzo hiyo
ya AFRIMMA imekuwa tuzo ya 30 kwa muimbaji huyo, idadi hiyo ilifahamika
rasmi baada ya kuandika ujumbe wa shukurani kwa mashabiki wake.Courtesy:matukio na vijana
Comments
Post a Comment